KOCHA Mkuu wa Yanga Mkongomani, Mwinyi Zahera amemtaja mwenyekiti mpya anayehitajika kuiongoza klabu hiyo. Hiyo ikiwa ni siku moja tangu Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) litangaze Machi 24, mwaka huu ndiyo siku ya uchaguzi huo.
Awali, uchaguzi huo ulisimamishwa na TFF baada ya kuzuiwa mahakamani na baadhi ya wanachama. Zahera alisema, mwenyekiti huyo anatakiwa awe na mipango thabiti ya kutafuta vyanzo vya mapato kupitia makampuni mbalimbali.
“Wanachama nawasikiliza wenyewe kila siku wanataka uchaguzi ufanyike, lakini shida inakuja wapo hao viongozi watakaoingoza Yanga kwa mafanikio.
“Hao viongozi wanaotaka kuiongoza Yanga, je wanafahamu hali ya kiuchumi iliyokuwepo kwenye timu, ni vema wakalifahamu kabla ya kuingia madarakani.
“Niwaambie Wanayanga wawe makini katika uchaguzi huo kwa kuweka viongozi watakaoiondoa klabu katika kipindi kigumu cha kiuchumi kwa sababu Yanga ni klabu kubwa yenye mtaji mkubwa wa mashabiki,” alisema Zahera.
0 Comments