NAHODHA na mshambuliaji tegemeo wa Simba, John Bocco amewaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo kwa kutamba kuwa wanawafunga wapinzani wao JS Saoura, Jumamosi nchini Algeria.
Bocco alisema, kocha wao tayari amewapa mbinu mbadala zitakazowapa ushindi katika mchezo huo wa kigeni.
“Tunajua umuhimu wa mechi hii ya ugenini tunayohitaji ushindi hivyo ni lazima tushinde ili tujiweke katika nafasi mzuri ya kusonga katika hatua inayofuata.
“Tutapambana kwa dakika 90 ili kuhakikisha wapinzani wetu tunawafunga ,”alisema Bocco.
Lakini Kocha wa Simba, Patrick Aussems amesisitiza kwamba kutokuwepo kwa Erasto Nyoni au Emmanuel Okwi wala hakuwezi kuwaathiri maana wapo mbadala wao.
0 Comments