Windows

YULE FUNDI UJENZI ALIYECHOTA SH MILIONI 31.8 ZA SPORTPESA HUYU HAPA




Na Mwandishi Wetu
FUNDI Ujenzi maarufu wa Buza, Kanisani jijini Dar es Salaam, Juma Mililu ameibuka mshindi wa Jackpoti Bonasi ya baada ya kujishindia Milioni 31, 858, 827 baada ya kufanikiwa kubashiri kwa usahihi mechi 12 kati ya 13.


Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mililu alisema alianza kubashiri na michezo hiyo ya kubashiri kupitia SportPesa, 2017 kabla ya juzi ushindi huo wake wa kwanza tangu ameanza kubashiri.


Mililu alisema, baada ya ushindi wa mamilioni hayo, amepanga kununua kiwanja na haraka ataanza ujenzi wa nyumba yake atakayoishi.


Mshindi huyo alisema, amepanga kuendelea na kubashiri na SportPesa baada ya kuvutiwa na kampuni hiyo jinsi inavyoendelesha michezo hiyo ya ubashiri.


“Niwashukuru SportPesa baada ya kunipatia fedha zangu za ushindi nilizozipata baada ya kubashiri mechi zangu 12 kati ya 13 kwa usahihi na kufanikiwa kujishindia fedha hizi.

“Kiukweli kabisa, SportPesa wapo makini na hawakawii kukutumia pesa zako mara baada ya kushinda ubashiri wako, hivyo ninafuraha sana moyoni kwangu iliyotokana na ushindi wangu.


“Baada ya ushindi huu nimepanga kuzitumia fedha zangu hizi kwa ajili ya kununua kiwanja na kuanza ujenzi wa nyumba yangu ya kuishi baada ya kukaa kwenye nyumba ya kukaa nyumba ya kupanga kwa muda mrefu.


“Niwashauri vijana wangu kubashiri matokeo yao kupitia SportPesa ambayo mimi nilianza kucheza nayo tangu mwaka 2017, hivyo baada ya ushindi huu nimepanga kuendelea kubashiri na SportPesa,”alisema Mililu.


 Mimi ni mama wa nyumbani tu ambaye sijishughulishi na kitu chochote, zaidi nipo nyumbani nalea familia yangu, hivyo baada ya ushindi huu nilioupata kwa kufanikiwa kushinda ubashiri wangu wa SportPesa.


Kwa upande wa SportPesa Mkurugenzi wa Uendeshaji. Luca Neghesti alimpongeza Mililu kwa ushindi huo wa Jackpoti Bonasi huku akimshauri kuendelea kubashiri na SportPesa ili ajishindie pesa zaidi.


“Kama SportPesa tunafarijika kuona jinsi huduma zetu zinawafikia watu waliokuwepo sehemu mbalimbali nchini na kubadili maisha yao hasa kwenye sekta ya kiuchumi nikimaanisha kuwawezesha kukuza mitaji yao na kujiendeleza kama familia.”




Post a Comment

0 Comments