Kutokana na mwenendo wa timu ya Yanga kuwa si mzuri kwa mechi za hivi karibuni, baadhi ya wanachama na wapenzi wa klabu hiyo wamesema wana wasiwasi wa kupata matokeo dhidi ya Alliance Machi 30, 2019.
Yanga itakuwa na kibarua cha mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Alliance tarehe tajwa hapo itakayochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Wanachama hao wameeleza kuwa ndani ya Yanga kuna mambo yamekuwa hayaendi sawa wakieleza kuwa hata uchaguzi haujafanyika hadi sasa.
Kutokana na hali hiyo wameshauri ni vema uchaguzi ukafanyika haraka ili kuziba nafasi za viongozi zilizo wazi ama uchaguzi mkuu ufanyike ili klabu iweze kuendeshwa vizuri.
Aidha wamefunguka kwa kusema wamekata tamaa na timu yao kwa ujumla na wana wasiwasi mkubwa wa kuchukua kikombe cha ligi mbele ya Simba kwa kuwa kuna vitu vingi ambavyo bado havijakaa sawa klabuni.
Wakati wanachama hao wakieleza hayo, tayari Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe, ametoa tamko la kuwataka Yanga kufanya uchaguzi huo ndani ya wiki mbili.
0 Comments