Mabingwa wa Ligi ya Kenya – KPL Gor Mahia watakutana na RS Berkane ya Morocco katika mtanange wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Africa kufuatia droo iliyofanywa Jumatano tarehe 20 Machi. Gor walicheza mara mbili na wapinzani wa Afrika Kaskazini Kaskazini katika hatua ya makundi, ambapo walishindwa na Na Hussein Dey ya Algeria na Zamalek ya Misri. Na sasa mara hii Gor wataelekea Morocco.
Gor Mahia ilikuwa timu ya kwanza kuwai kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo wakati ilibwaga Petro Atletico ya Angola katika mchuano wa mwisho wa Kundi D.
Wataanza nyumbani katika mchuano wa ufunguzi dhidi ya RS Berkhane Aprili 7 kabla ya kuelekea Morocco Aprili 14 kwa mchuao wa marudio.
Kama watashinda, Gor bado wataelekea Afrika Kaskazini kwa nusu fainali, kwa sababu kwenye droo yao, timu ya Zamalek ya Misri na Hassania Agadir zitakabana koo katika robo fainali nyingine.
Katika mechi nyingine, Nkana FC ya Zambia itakabana koo na CS Sfaxien ya Tunisia. ESS ya Tunisia itakwaruzana na miamba wa Sudan Al Hilal katika robo fainali nyingine.
0 Comments