VIONGOZI waliopo madarakani katika Klabu ya Yanga wanatakiwa kuachia ngazi ili kupisha mchakato wa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika wakati wowote kuanzia sasa mara baada ya mkutano mkuu wa wanachama kufanyika.
Klabu ya Yanga ipo katika mchakato wa kufanya uchaguzi mkuu wa viongozi baada ya ule wa awali kusitishwa uliokuwa ufanyike Januari 13, mwaka huu kufuatia baadhi ya wanachama kwenda kupinga mahakamani.
Aidha hivi karibuni, Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa klabu hiyo, George Mkuchika alieleza hatima yao ya kutaka kuitisha mkutano wa dharura wa wanachama ili kujadili suala hilo.
Taarifa iliyozifi kia Championi Jumamosi zinaeleza kuwa, viongozi wote waliopo madarakani hivi sasa wanatakiwa kujiuzulu ili kupisha mchakato huo kwa kupata viongozi wapya.
Yanga imefi kia hatua hiyo baada ya viongozi waliokuwa madarakani akiwemo mwenyekiti, Yusuf Manji kujiuzulu, hivyo kusababisha kubakiwa na viongozi wanne wa kuchaguliwa huku waliobakia wakikaimu nafasi mbalimbali.
“Uamuzi ambao umefi kiwa katika vikao vilivyofanyika hivi karibuni ni kwamba viongozi wote walio madarakani wajiuzulu ili kupisha uchaguzi kufanyika ili kupata viongozi wapya. “Maamuzi hayo yatafanyika mara baada ya mkutano mkuu wa dharura utakaofanyika hivi karibuni ambao unaandaliwa,” alisema mtoa taarifa huyo.
Championi lilimtafuta Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Siza Lyimo, kuzungumzia suala hilo alisema: “Siwezi kusema chochote atafutwe kaimu mwenyekiti (Samwel Lukumay) ndiye mwenye nafasi ya kulizungumzia suala hilo.” Championi lilimtafuta Lukumay ambaye alisema hawezi kuzungumza chochote kuhusiana na ishu hiyo.
Viongozi waliojiuzulu ni aliyekuwa mwenyekiti Manji, Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga na wajumbe Inspekta Hashim Abdallah, Salum Mkemi, Omary Said, Ayoub Nyenzi, Thobias Lingalangala na aliyekuwa Katibu Mkuu, Boniface Mkwasa.
Waliopo madarakani mpaka sasa ni, Samuel Lukumay ambaye ni kaimu mwenyekiti, Siza Lyimo (kaimu makamu mwenyekiti) na Hussein Nyika yeye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili.
CHANZO: CHAMPIONI
0 Comments