Windows

Bao la dakika ya mwisho la Reus laiweka Dortmund kileleni

Bao la nahodha wa Borussia Dortmund Marco Reus katika dakika ya mwisho lilikamilisha mechi ya kusisimua ya iliyoshuhudia mabao matano dhidi ya Hertha Berlin iliyomaliza mechi na wachezaji 10 katika dimba la Olympiastadion.

Marco Reus amekuwa nguzo muhimu katika kikosi cha BVB

Ushindi huo wa Dortmund wa 3-2, unaiweka kileleni mwa ligi na pengo la pointi tatu.

Dortmund walilazimika kutoka nyuma. Mara mbili kupitia mabao ya Thomas Delaney na Dan-Axel Zagadou ambayo yalifuta mabao mawili ya kipindi cha kwanza kutoka kwa Salomon Kalou, ambapo la pili lilikuwa kupitia penalti.

Baada ya mchezaji wa Hertha Jordan Torunarigha kutimuliwa uwanjani katika dakika ya 85, wageni waliongeza mashambulizi huki Reus akifunga bao lake la 19 msimu huu na kuwapa ushindi wa 3-2

Timo Werner alimaliza kiu yake ya kufunga mabao

Schalke, ambao walimtimua kocha mkuu Domenico Tedesco na naibu wake Peter Perchtold siku ya Alhamisi baada ya kichapo cha 7-0 na Manchester City katika Champions League, ilipoteza mechi ya sita mfululizo katika mashindano yote baada ya kuzabwa 2-1 na RB Leipzig.

Chini ya kaimu kocha Huub Stevens, ambaye ameifundisha klabu hiyo mara mbili huko nyuma, Schalke ilishindwa kujikwamua baada bao la dakika ya 14 la Timo Werner lake la 12 msimu huu.

 


Post a Comment

0 Comments