Windows

UJANJA WA SIMBA KIMATAIFA UPO HAPA, ROBO FAINALI KAZI IPO



LICHA ya kutinga kibabe hatua ya robo fainali, kikosi cha Simba kimeishangaza Afrika kutokana na aina ya matokeo iliyokuwa ikiyapata.

Simba imefuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuwatungua AS Vita mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, wikiendi iliyopita.

Kwenye michezo 10 ambayo Simba wamecheza kuanzia hatua ya awali mpaka  makundi,  walifanikiwa kupata ushindi kwenye mchezo mmoja tu wa ugenini, huku mingine minne wakipoteza.

Ushindi huo ni dhidi ya Mbabane ya Eswatini ambapo Simba ikiwa ugenini ilishinda 4-0, huku nyumbani ikishinda 4-1.

Simba walianza kupokea kichapo mbele ya Nkana FC kwa kufungwa mabao 2-1, ila waliporejeana Uwanja wa Taifa, Nkana walifungwa mabao 3-1.

 Kichapo kingine walipokea mbele ya AS Vita mabao 5-0, kabla ya kushinda wao mabao 2-1 nyumbani.

Al Ahly nayo iliifunga Simba 5-0 kule Misri, lakini Dar ikafungwa 1-0, huku JS Saoura nayo hapa Dar ilifungwa 3-0 na kwao ikashinda 2-0.

Takwimu zinaonyesha kuwa, katika mechi hizo kumi, Simba imefunga mabao 13 Uwanja wa Taifa na ugenini imeruhusu mabao 14.

Katika timu zilizofuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo, Simba pekee ndiyo iliyoruhusu mabao mengi mpaka sasa.

Kinara wa mabao kwa sasa ndani ya Simba ni Meddie Kagere ambaye anayo sita akiwa amefunga matano Uwanja wa Taifa na moja nje ya Tanzania, akifuatiwa na Clatous Chama mwenye mabao matano ambayo matatu ameyafungia Uwanja wa Taifa na mawili nje ya uwanja huo.

Hatua ya robo fainali baada ya droo kuchezwa tayari wameshatambua mbaya waoa atakuwa ni nani kwa sasa.

Simba watamenyana na TP Mazembe ya nchini Congo ambayo ushindani wake mkubwa kwenye ligi yao ni dhidi ya AS Vita ambao wamesharejea Congo na maumivu ya kunyoohswa na Simba Taifa.

Kwa sasa Simba inabidi ichange karata yake vema kwani hapa ni mwendo wa hesabu tu kwenye hatua hii ili kutinga hatua ya nusu fainali.

Kwa mujibu wa kocha wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa anatambua hatua ya robo fainali ni ngumu ila atakaa chini kuweza kuja na mbinu ambazo zitampa matokeo hata akitoka nje ya nchi.

Hivyo kwa sasa ni muda muafaka kwa Simba kujipanga upya kwenda na kasi iliyopo kwenye michuano hii ambayo ni mikubwa Afrika.

Post a Comment

0 Comments