Windows

TUNALIA NA ZAHERA AKIWA KATUPELEKA DARASANI


Kumekuwa na malalamiko ya Kocha Mwinyi Zahera kwamba aliaga anarejea kwao DR Congo katika majukumu ya timu ya faida.

Akaicha Yanga ikisafiri kwenda katika majukumu dhidi ya Lipuli FC mjini Iringa.

Baadaye ametuhumiwa kuendelea kubaki jijini Dar es Salaam kuisaidia AS Vita inayofundishwa na rafiki yake Ibenge ili iimalize Simba kwenye mechi ya mwisho hatua ya makundi kwenda robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

KAMA NI KWELI Zahera kafanya hivyo ni kosa maana atakuwa si mkweli kwa Wanayanga lakini atabaki kuwa sehemu wa shujaa wa taifa lake kama Vita Club itasonga mbele au la.

Maana Zahera achana na urafiki na bosi wake Ibenge lakini atakuwa MTAIFA na anajua faida ya Vita Club kusonga mbele kwa DRC. Zahera ANALAUMIWA sawa lakini ANATUFUNDISHA.

JITAFAKARI wewe Mtanzania unayetaka kufa kwa jazba, presha eti Vita Club ya DR Congo?

Jifunze kwa Zahera ambaye angeweza kujivunia Simba inatoka Tanzania eneo analofanyia kazi na anaishi na Watanzania walio Yanga na Simba. SEMBUSE WEWE hupajui Congo wala hakuna anayejukujua kule unataka KUONYESHA una machunguuuuuu.

Si lazima kuishabikia timu Ila jifunze unatakiwa kufanya hata kama huelewi kabisa linapofikia suala la UTAIFA.

Na Saleh Ally


Post a Comment

0 Comments