Timu ya taifa ya Tanzania – Taifa Stars imeendelea kujinoa kuelekea mchezo uliobeba historia ya Watanzania dhidi ya Uganda, The Cranes mtanange utakaofanyika dimba la Mkapa Machi 24 Jumapili kuanzia saa 12 jioni.
Taifa Stars kuelekea mtanange huo hamasa ni kubwa sana nje mpaka ndani ya uwanja, kunaonekana kuwa na hamasa kubwa kutokana na kazi kubwa anayofanya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ambaye ni Mwenyekiti wa Saidia Taifa Stars ishinde.
Asilimia kubwa ya mashabiki walikuwa wadogo kipindi Tanzania inafuzu miaka hiyo ambapo sasa mashabiki wanahitaji kuwa sehemu ya kushuhudia Tanzania ikifuzu kwenda AFCON kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1980 ambapo iliingia mara ya mwisho kupitia goli la Peter Tino.
Kamati ya Saidia Taifa Stars ishinde imejipambambanua katika uwanda mpana ambapo mbali na kujenga uelewa wa mechi hii, ahadi mbalimbali zimetolewa kwa lengo la kufanya kila shabiki kuwa sehemu ya mchezo huo.
Tanzania mwenye alama 5 kujikatia tiketi ya kwenda Misri AFCON inahitaji alama tatu na kuiombea Lesotho yenye alama 5 kupoteza, hata sare dhidi ya Cape Verde 4, au Cape Verde ishinde, Taifa Stars itakuwa imefuzu. Uganda ina alama 13 tayari imeshakata tiketi ya michuano hii ikiwa ni mara ya pili mfululizo.
Tanzania Taifa Stars itakosa huduma ya Mlinda mlango Aroni Kalambo ambaye amepata maumivu madogo yaliyomuondoa katika maandalizi ya mwisho ya kikosi kilicho chini ya Amunike.
Mechi hii ya mwisho kundi L itafanyika mda mmoja na ile ya Lesotho dhidi ya Cape Verde wakati ambapo hapa Tanzania kiingilio kitakuwa 2000 kwa mzunguko.
0 Comments