Windows

SOLSKJAER KUWAUZA SANCHEZ, ROJO NA VALENCIA


KAIMU meneja (kocha) wa klabu ya Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer,  anawataka wachezaji Alexis Sanchez, beki wa Argentina Marcos Rojo, 29, na beki wa kulia wa Ecuado Antonio Valencia, 33, kuondoka katika klabu hiyo mwisho wa msimu huu.

Solskjaer ambaye alichukuliwa na klabu hiyo kama zoezi la muda, hivi sasa anaonyesha ni jambo la muda tu kuweza kujichimbia katika nafasi hiyo moja kwa moja.

Hili linajidhihirisha pale Solskjaer  (46) alipokutana na  mmiliki mwenza wa klabu hiyo,  Avram Glazer, mwezi uliopita na anapokuwa na mawasiliano ya kila siku na Mwenyekiti Mtendaji wa klabu hiyo,  Ed Woodward.

Wiki hii, Solskjaer alitoa ishara ya wazi zaidi kwamba ataendelea kuisimamia klabu hiyo msimu ujao pia, akikiri kabisa kwamba bado hajaanza kutazama sehemu nyingine ya kwenda kufanyia kazi.

“Ni wazi kwamba sasa nafanya kazi kama vile nitaendelea kuwa hapa.  Ninaifikiria klabu hii mnamo miaka mitano na kumi ijayo,” alisema.

Ni katika mazingira haya, Solskjaer amempa kabisa Woodward orodha ya wachezaji anaotegemea kuwa nao msimu ujao, ikiwa ni pamoja na nyota wa Uingereza anayechezea klabu ya Dortmund ya Ujerumani,  Jadon Sancho.

Licha ya Dortmund kusema mchezaji huyo atabaki uwanja wa Westfalenstadion, gazetila Mirror Football limesema United wako radhi  kuvunja benki na kulipa fedha yoyote kubwa zaidi ili wampate mchezaji huyo kwa ajili ya ligi kuu ya Uingereza, Premier League,  msimu ujao.

Post a Comment

0 Comments