UONGOZI wa timu ya Singida United umesema kuwa umeshamalizana na aliyekuwa kocha mkuu, Dragan Popadic na leo anatarajiwa kusepa mazima huku akiacha mikoba yake mikononi mwa Felix Minziro.
Ofisa Habari wa Singida United, Cales Catemana amesema kuwa tayari mipango yote imekamilika na zile kelele zilizokuwa ndani ya timu zimetulia kwani Popadic alikuwa akiongozwa na mihemuko ndani ya timu.
"Tumeshamalizana naye kila kitu na Popadic hivyo kwa sasa timu ipo chini ya Minziro ambaye naye ameshapewa mkataba kutokana na ubora wake hivyo tunaamini atafanya kazi kwa umakini na kuifanya Singida United kuwa ya ushindani.
"Kwa sasa timu ipo kambini ikijiaanda na mchezo wa shirikisho dhidi ya Lipuli hivyo hakuna namna nyingine ambayo kwa sasa wapinzani wetu watatoka kwani tuna uzoefu na mashindano haya na tutaleta ushindani kwa wapinzani wetu," amesema Katemana.
Singida United watamenyana na Lipuli Jumatano ya wiki ijayo Uwanja wa Samora uliopo mkoani Iringa ikiwa ni hatua ya robo fainali.

0 Comments