Windows

Simba yamwagiwa fedha na Sportpesa

Klabu ya Simba imemwagiwa fedha na Kampuni ya Kubashiri matokeo Sportpesa baada ya kufanikiwa kuingia hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika wiki hii kwa kuitoa AS Vita kutoka Congo.

Simba imepokea kitita cha shiingi milioni 50 ikiwa sehemu ya mkataba ambao Kampuni hiyo iliingia miaka miwili iliyopita, ambapo kila hatua Simba watakayovuka kiasi cha fedha kinaongezeka mara mbili.

Akizungumza na Waandishi wa Habari wa michezo Tanzania, Mkurugenzi Mtendaji wa Sportpesa Abasi Tarimba amesema “tunaamini kufanikiwa kwa Simba kumechagizwa na pesa tulizowekeza kwao”.

“Tunaishukuru Simba kwa kufanya vizuri mbali na kuiwakilisha Tanzania vyema lakini pia inaikuza Kampuni yetu, kutokana na hilo tunatoa kitita cha milioni 50 kama sehemu ya mkataba wetu na wao (Simba),” amesema Tarimba ambaye amewai kuwa na Uongozi katika klabu ya Yanga.

Mbali na fedha za Sportpesa, Simba imefanikiwa kuchukua kitita cha milioni 1.5 kutoka kwa CAF kama sehemu ya faida ya kufuzu hatua hiyo.

Ikumbukwe tu Simba imefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali baada ya kuifunga AS Vita goli 2-1 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, na kuwa mara ya kwanza baada ya zaidi ya miaka 23.

Aidha, ratiba ya robo fainali imepangwa leo Machi 20 ambapo klabu ya Simba itakutana na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo


Post a Comment

0 Comments