Hatimaye wahenga husema “Siku ya deni haikawii kufika” Baada ya kusubiri kwa takribani siku nne kujua nani atapangwa na Simba kutoka Tanzania kwenye hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika sasa mambo yamewekwa hadharani.
Simba itavaana na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika hatua hiyo, huku rekodi nzuri waliyo nayo mbele ya Simba ikitoa unafuu kwa upande wao.
Katika droo ya leo, mkondo wa kwanza utapigwa April 5/6 ambapo Simba itakuwa mwenyeji wa mchezo huo kabla ya mkondo wa pili kati ya tarehe 12/13 huko Kinshasa Congo.
Hii itakuwa mara ya pili kwa klabu ya Simba kukutana na TP Mazembe katika Ligi ya Mabingwa huku michezo yote Simba ikiishia kuangukia pua.
Mbali na kupoteza kwa Simba bado ilifanikiwa katika mauzo ya wachezaji ambapo Mbwana Ally Samatta alijiunga na timu ya Mazembe ikiwa hatua ya mwanzo ya mafanikio yake.
Kwa timu zilizofuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa, TP Mazembe ni timu inayoongoza kufunga magoli mengi mpaka sasa ambapo imefunga jumla ya 13 wakati Simba ikiwa timu pekee iliyofunga magoli machache 6 pekee na kufungwa 13.
Droo ya mechi zingine ipo kama hivi:
.CS Constantine itacheza na Esperance De Tunis (Tunisia)
.Horova dhidi ya Wydad Casablanca (Morocco).
. Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini) itamenyana dhidi ya Al Ahly kutoka Misri.
Mechi zote mkondo wa kwanza zitachezwa kwenye tarehe 5 au 6 katika mwezi April mwaka huu.
0 Comments