

Imeelezwa kuwa Singida United imejutia kusajili nyota wanaotoka klabu za Simba na Yanga wakidai wao ndio chanzo cha migogoro ndani ya timu yao.
Chanzo kimeeleza Singida United wamekuwa na msimu mbaya mwaka huu wa kushika nafasi ya tatu kutoka mkiani kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wakiwa na pointi 33 wakicheza michezo 30.
Taarifa imeeleza Mkurugenzi wa Singida United, Festo Sanga, alisema kufanya vibaya kwa timu hiyo kumetokana na kusajili wachezaji wengi kwa gharama kubwa.
Sanga amesema gharama hizo zimewafanya kushindwa kumudu matumizi na kujikuta wakijiendesha kwa tabu.



0 Comments