Na Saleh Ally, Antalya
Kikosi cha Serengeti Boys, leo kimerejea mazoezini kujiandaa na mechi yake dhidi ya wenyeji Uturuki.
Kikosi hicho kipo hapa mjini Antalya kushiriki michuano ya Uefa Assist yanayoendelea na tayari timu imecheza mechi mbili na kushinda moja na kupoteza moja.
Walianza kwa kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Guinea kabla ya kuamka katika mechi ya pili na kuwanyoosha Australia kwa mabao 3-2 katika mechi ya pili.
Katika mazoezi ya leo, Serengeti Boys walifanya yale mepesi lakini pia wakajifunza mbinu kadhaa katika umaliziaji pia ulinzi.
Kesho, Serengeti Boys, inashuka dimbani kuwavaa wenyeji Uturuki na hii itakuwa mechi yao ya mwisho ya michuano hiyo ya Uefa Assist.
0 Comments