Windows

KOCHA STAND AKATAA BAO MBILI ZA SIMBA 'MWAMUZI ALIWASAIDIA'


Kocha Msaidizi wa Stand United, Athuman Bilali 'Bilo' amemtupia lawama Mwamuzi wa mechi ya jana dhidi ya Simba waliyochapwa kwa mabao 2-0.

Akizungumza mara baada ya mchezo, Bilo alieleza kuwa Mwamuzi aliwabeba na kuwasaidia Simba kupata mabao 2 ambayo alidai hayakuwa halali.

Kocha huyo ambaye alitamba kuwamaliza Simba kwenye kipute hicho, anaamini Mwamuzi aliwapa msaada Simba na mechi haikuwa na usawa kiuchezeshaji.

"Tumefungwa lakini Mwamuzi amewasaidia Simba, si mabao sahihi kwakuwa kulikuwa na upendeleo kwao",

"Naweza kusema msaada wa refa umewasaidia Simba kuchukua alama tatu ambazo si halali kutokana na namna mchezo ulivyochezeshwa" alisema.

Post a Comment

0 Comments