Windows

Hakika Yanga ni timu ya Wananchi,yaja na mpango huu kabambe.

HAKIKA timu ya Yanga ni timu ya wananchi ndivyo naweza kusema baada ya timu hiyo kuja mpango wa kuwaangukia mashabiki wa timu hiyo katika kufikia malengo mbali mbali ya kuivusha timu hiyo katika kipindi hiki .

Mwenyekiti wa kamati ya uhamasishaji kwa ajili ya kuichangia Yanga, Antony Mavunde amesema mipango iliyopo kwa sasa ambayo ni kufanikiwa kuchangia zaidi ya shilingi 1.5 bilioni kutoka wa wanachama na mashabiki wa Yanga mikoa yote nchini.

amewataka wananchi kuendelea kuichangia timu ili kufikia malengo ambayo wamejiwekea.

Yanga kwa sasa inajiendesha kutokana na nguvu ya michango ya wanachma kutokana na kupita kipindi cha mpito.

Ili kuichangia Yanga kupitia mitandao ni kupitia namba hii *150*01# kisha chagua namba 4 lipa bili, hatua inayofuata chagua namba 3 weka namba ya kampuni ambayo ni 101120, kumbukumbu namba weka namba 1 kisha weka kiasi kisipungie mia tano, weka namba ya siri kuhakiki kisha utapokea Ujumbe wa kuthibitisha.


Post a Comment

0 Comments