

Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amesema hana nia mbaya kuwa karibu na timu ya AS Vita kama ambavyo Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amekuwa anadai.
Zahera ameeleza uwepo wake wa karibu na Vita ni kwa sababu timu hiyo ina wachezaji takribani watano wanaoichezea timu ya taifa ya Congo.
Kocha amesema asitafsiriwe vibaya kwani wale ni sawa na ndugu zake na muda mwingi anakuwa haonani nao kutokana na kubanwa na majukumu ya kazi.
Kutokana na sintofahamu juu yake, Zahera amemtaka Manara asianze kumlaumu kwani hawezi kufanya lolote baya kuelekea mechi yao ya kesho na Vita kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
"Unajua ile timu ina wachezaji takribani watano wanacheza timu ya taifa, ninawafundisha, sina ubaya wowote na yale anayoyasema Manara.
"Asinitafsiri vibaya kwani si vibaya kwenda kusalimiana nao maana ni ndugu zangu, ni wakongo wenzangu.
CHANZO: EFM




0 Comments