BAADA ya kikosi cha Azam FC kuwa chini ya kocha Idd Cheche wengi wanapenda kumuita Ole Gunnar amevunja rekodi ya bosi wake wa zamani Hans Pluijm kwa kufunga mabao mengi mara mbili zaidi ya Mholanzi huyo.
Mpaka sasa Cheche ameongoza Azam kupata ushindi kwenye mechi tatu za ligi na moja ya kwenye Shirikisho iliwapa nafasi ya kufuzu hatua ya robo fainali.
Cheche amekusanya jumla ya mabao 16 kwenye michezo minne ambayo ni sawa na wastani wa mabao 4 kwenye kila mchezo ambao wameshuka Uwanjani kwa sasa wakati Pluijm alikusanya mabao 6 kwenye mechi nne za mwanzo.
Cheche alishinda dhidi ya Lyon Uwanja wa Uhuru kwa mabao 3-1, ikiwa ni mchezo wa ligi na akashinda mchezo wa Shirikisho dhidi ya Rhino Rangers Uwanja wa Chamazi mabao 3-0, kabla ya kuinyoosha JKT Tanzania mabao 6-1 na juzi kumaliza kwa Singida United kwa ushindi wa mabao 4-0.
Pluijm kwenye michezo yake minne ya awali alikusanya jumla ya mabao sita ikiwa ni michezo ya ligi na michezo hiyo ilikuwa dhidi ya Mbeya City 0-2, Ndanda 0-3, Alliance 0-1 na alitoka sare na Lipuli, michezo yote Uwanja wa Chamazi.
Azam ipo nafsi ya pili baada ya kucheza michezo 28 imejikusanyia jumla ya pointi 59 kibindoni kwa sasa.
0 Comments