Rais wa Bayern Munich Franz Beckenbauer anaamini kuwa taji la msimu huu la Bundesliga litaamuliwa katika mtanange wa nyumbani wa mabingwa hao dhidi ya vinara wa sasa Borussia Dortmund.
Dortmund inaongoza msimamo wa ligi kwa tofauti ya mabao baada ya Bayern kupambana na kuziba kabisa mwanya wa pointi tisa uliokuwepo katika wiki za karibuni. Beckenbauer anaamini kuwa kutetea ubingwa wa Bundesliga msimu huu yatakuwa mafanikio makubwa kuliko kushinda Ligi ya Mabingwa kwa Bayern.
“Ubingwa wa Bundesliga kwa maoni yangu utaamuliwa Aprili 6 katika mpambano wa moja kwa moja dhidi ya Dortmund na kwangu mimi ndio taji lenye thamani Zaidi,” Beckenbauer mwenye umri wa miaka 73 ameliambia gazeti la Bild.
Kuna mechi 10 zilizosalia katika Bundesliga. Bayern watawaalika Liverpool wiki ijayo katika mechi yao ya mkondo wa pili wa hatua ya 16 za mwisho ya Champions League huku matokeo yakiwa 0 – 0 kutokana na mkondo wa kwanza.
0 Comments