Windows

Bayern yavunja rekodi kwa kumsaini Hernandez

Bayern Munich wamesaini beki wa Atletico Madrid Lucas Hernandez kwa mkataba wa miaka mitano kwa kima cha euro milioni 80, ambayo ni rekodi ya usajili kwa klabu hiyo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, ambaye alishinda Kombe la Dunia 2018 na Ufaransa, atajiunga na vinara hao wa Bundesliga mnamo Julai mosi.

Wakati akifanyiwa vipimo vya matibabu katika Bayern, madaktari waligundua kuwa alikuwa na majeraha ya mishipa kwenye goti lake la kulia na hivyo akafanyiwa upasuaji Jumatano. “Hii ni mojawapo ya siku muhimu katika kazi yangu ya kandanda,” Alisema Hernandez.

Mfaransa huyo ambaye anaweza kucheza kama beki wa kati na beki wa kushoto, ameichezea Atletico mechi 67 za La Liga na kushinda Europa League na Super Cup.

Ameichezea Les Bleus ya Ufaransa mara 15, ambapo alishiriki katika mechi zote za Kombe la Dunia nchini Urusi.


Post a Comment

0 Comments