Alliance bado wana maumivu ya kunyooshwa bao 1-0 kwenye mchezo wao wa ligi uliochezwa kwenye Uwanja huo wamepania kulipa kisasi kwenye mchezo wao wa Shirikisho.
Ofisa Habari wa Alliance, Jackson Mwafulango amesema mipango ipo sawa na wataweka kambi nchini Rwanda kwa muda wa wiki moja ili kuwa kwenye hali ya utulivu kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Yanga.
"Tunawatambua wapinzani wetu vizuri, tumecheza nao hapa kwenye Uwanja wetu kwa kuwa wanatufuata tena tunakwenda kuweka kambi Rwanda kwa muda tukirejea tutakuwa na kitu cha kipekee kwenye mchezo wetu.
"Kila kitu kinakwenda sawa ni jambo la muda tu kuona namna ambavyo tutapata matokeo, morali na maandalizi kwa wachezaji kwa sasa yanakwenda sawa," amesema Mwafulango.
0 Comments