

Na George Mganga
Mbunge wa Jimbo la Ilala, Dar es Salaam, Mussa Azzan Zungu, ameitaka serikali kuvifanyia marekebisho viwanja haswa vya mikoani ili kuzipa wepesi timu kushindana vizuri.
Kauli ya Zungu imekuja kufuatia timu ya Yanga kwenda suluhu dhidi ya Singida United katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa wiki hii mjini Singida.
Zungu ameutaja Uwanja huo ambao ulitumika kuwa na mapungufu mengi ikiwemo PICHI yake kuwa na matatizo na akiamini ilisababisha matokeo kutokuwa kama ilivyopaswa.
Ameeleza kuwa aliionea huruma Yanga kucheza mechi yake katika Uwanja kama ule ambao uliwapa wakati mgumu kupata matokeo.
Kutokana na changamoto hiyo, Zungu ameitaka serikali ambayo inamiliki viwanja vingi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuangalia namna ya kuvifanyia maboresho ili viendane na hadhi ya Ligi Kuu Bara.
"Kwa Uwanja kama ule kwa Yanga kuchezea ni aibu, hauendani na hadhi ya ligi yetu, naiomba serikali kupitia CCM ifanye namna ili maboresho yafanyike haraka na timu zicheze vizuri" alisema.



0 Comments