

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema yupo tayari kufanya kazi klabuni hapo bila malipo, imeelezwa.
Taarifa imeeleza kuwa Zahera ameshawahi kufanya kazi sehemu tofauti bila kutegemea malipo hivyo haoni tatizo kwake endapo akifanya hivyo Yanga.
Zahera ambaye amewahi kusema timu yao inapitia wakati mgumu, ameeleza kuwa amekuwa akitoa hata fedha zake kwa ajili ya kuisaidia klabu haswa kipindi hiki cha mpito.
Kocha huyo amefunguka kuwa hategemi mshahara kuendesha maisha yake kwani ana biashara nyingi ambazo anazifanya.
Kwa moyo huo, Zahera ana imani kuisaidia Yanga kutaongeza morali kwa timu na wachezaji kwa ujumla kwani mshahara kwake si ishu na yupo tayari kufanya akzi hiyo bila kulipwa kwa miaka mingi.




0 Comments