Windows

YANGA YAANZA HARAKATI ZA KUMALIZANA NA MCHEZAJI WAKE HARAKA KABLA HAJACHUKULIWA NA SIMBA


Uongozi wa klabu ya Yanga umeanza mikakati kabambe ya kuboresha mkataba wa mchezaji wake, Mshambuliaji Ibrahim Ajibu ambaye ameanza kuhusisha kurejeshwa Simba, imeelezwa.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinasema hivi sasa kinachoumiza ni kuona namna gani mabosi hao wanafanikisha mipango ya kumbakisha mchezaji huyo fundi.

Kutokana na Yanga kuwa kwenye wakati wa mpito hivi sasa, kuna namna inafanyika ili kupata fedha za kuongeza mkataba wake ili asiondoke na akaelekea alipotokea.

SImba ambao wametoka kuiangamiza Yanga jana kwa bao 1-0 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, inaelezwa wameshaanza harakati za kimyakimya kumalizana naye mapema baadaye.

Simba wanaonesha dhahiri shahiri bado wanamkubali Ajibu kutokana na kiwango chake hivyo endapo Yanga watazubaa anaweza akarejeshwa Unyamani.'

Wakati huo Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera, amezidi kuwaasa Yanga wafanye kila liwezekanalo ili kumbakiza nyota huyo.

Taarifa zinasema Zahera bado anamkubali zaidi mchezaji huyo na anahitaji zaidi huduma yake kwani amekuwa na msaada mkubwa zaidi kikosini.

Takwimu zinaonesha Ajibu tangu ajiunge na Simba misimu miwili iliypita amefunga jumla ya mabao 13.


Post a Comment

0 Comments