MEDDIE kagere mshambuliaji wa Simba jana dakika ya 71 akimalizia pasi ya Bocco alibadilisha mambo manne kwa wakati mmoja baada ya kufunga bao la ushindi Uwanja wa Taifa.
Kagere alibadilisha matokeo kwa kuipa pointi tatu muhimu timu yake na kuifanya ifanikiwe kushinda mchezo wake wa ugenini na kuwa na pointi 39 kutoka 36.
Matokeo hayo pia jambo la pili ni kuifanya Simba ipande kwa nafasi mbili kutoka nafasi ya tano mpaka kufikia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi.
Jambo la tatu ni kuongeza idadi ya mabao ya kufunga awali Kagere alikuwa na mabao nane na sasa anafikisha mabao tisa.
Jambo la nne ni kuongeza idadi ya michezo kwa Yanga ya kupoteza kwani katika michezo yao ya awali walifungwa mchezo mmoja kati ya michezo 23 na jana wanafikisha mchezo wa pili kupoteza.
0 Comments