Windows

YANGA KUTUMIA MBINU MPYA KUPATA USHINDI UGENINI


Mwinyi Zahera, Kocha mkuu wa Yanga ambaye anamwani mlnda mlango kinda Ramadhani Kabwili amesema kazi yake ya kwanza ilikuwa kuwaondoa hofu ya ugumu wa mechi za kanda ya ziwa wachezaji wake.

Zahera amesema wachezaji wamekuwa wakishindwa kupata matokeo wakati mwingine kutaokana na hofu wanayojiwekea juu ya ugumu wa mechi za kada ya ziwa hali iliyofanya awape mbinu mpya.

"Nimewafundisha mbinu nyingi wachezaji wangu na tulipokuwa kwenye mazoezi nimewaambia namna ambavyo wanatkiwa kufanya.

"Najua kazi ni ngumu ndio maana nimeanza na kuwaambia wachezaji kwamba ni kitu cheesi kushida ukiwa ugenini, leo tutafanya kazi ya ziada kupata matokeo ugenini," amesema Zahera.

Yanga ni kinara wa ligi akiwa na pointi 58 baada ya kucheza michezo 24 amepoteza michezo miwili pekee mpaka sasa. 

Post a Comment

0 Comments