Windows

MBELGIJI WA SIMBA AMFIKIRIA PLUIJM WA AZAM FC


PATRICK Aussems, Kocha mkuu wa Simba ameanza kumpigia hesabu mpinzani wake Hans Pluijm raia wa Uholanzi kabla hawajukatana Ijumaa.

Aussems amesema maandalizi ya kikosi chake si kwa ajili ya mchezo mmoja bali ni michezo yake yote iliyo mbele ambayo anafikiria mbinu mpya zitakazompa ushindi.

"Nina michezo mingi kwa sasa ambayo ni ya mzunguko wa kwanza najua nitakutana na Azam FC, Lipuli pamoja na Mtibwa, yote nafikiria namna mpya itakayonisaidia kupata matokeo.

"Wachezaji wanajua majukumu yao na kukosea inatokea kwenye mchezo kama ambavyo tunakabiliwa na michezo mingi nasi tunatikiwa tuwe tofauti," amesema Aussems.

Ushindi wa jana mbele ya African Lyon unawarejesha nafasi ya tatu wakiwa na pointi 42 baada ya kucheza michezo 17.


Post a Comment

0 Comments