LEO saa 10:00 jioni, Uwanja wa Mkapa nyasi zitawaka moto kwa kuwakutanisha mafahari wawili ambao vita yao kubwa ni kuishusha Yanga kileleni.
Huu ni mchezo wa kwanza kwa wapinzani hawa kukutana msimu huu wa mwaka 2018/19 huku mwenyeji wa mchezo akiwa ni Azam FC.
Mpaka sasa tangu Azam FC ipande daraja msimu wa mwaka 2013/14 na kushiriki Ligi Kuu Bara imekutana na Simba mara 10.
Katika michezo yote hiyo hakuna mbabe hata mmoja ambaye ameweza kumuonea mwenzake kwa kumfunga mabao mengi zaidi wote wameishia kufungana mabao 2 ama bao moja.
Wote wawili wametoa sare mara nne na kila mmoja ameshinda mara tatu hali ambayo inaonyesha ushindani ni mkubwa zinapokutana timu hizi.
Zilipokutana kwenye mismu yao mitano iliyopita Ligi Kuu Bara matokeo yao yalikuwa hivi:-
2013/14
Simba 1-2 Azam FC
Azam FC 2-1 Simba
2014/15
Azam FC 1-1 Simba
Simba 2-1 Azam FC
2015/16
Azam FC 2-2 Simba
Simba 0-0 Azam FC
2016/17
Azam FC 0-1 Simba
Simba 0-1 Azam FC
2017/18
Simba 1-0 Azam
Azam 0-0 Simba
2018/19 ?
Leo ndo atajulikana nani mbabe ambaye ataanza safari ya kumkibiza kinara Yanga mwenye pointi 61, Azam wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi 50, Simba nafasi ya tatu pointi 42.
0 Comments