Uongozi wa klabu ya Yanga umekubali matokeo ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Licha ya kupoteza mechi hiyo, Yanga wameeleza kuwa haina maana kufungwa na Simba ndiyo wamepoteza mbio za ubingwa kwani bado mechi zinaendelea.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, amesema hawajapoteza ligi bali wamepoteza mechi pekee, na haya ndiyo aliyoandika.
0 Comments