Windows

BEKI WA SIMBA ZANA, ANAYEPANDA NA KUSHUKA AWAZIDI KETE MASTAA HAWA WA YANGA


ZANA Coulibaly wa Simba amewazidi kete mastaa wa Yanga, Haruna Moshi ‘Boban’ na Mohammed Issa ‘Banka’.

 Wachezaji hao wote walisajiliwa kwenye dirisha dogo isipokuwa Banka alisajiliwa dirisha kubwa ila alikuwa na adhabu aliyopewa na Shirikisho la Soka la Dunia (Fifa) kwa muda wa miezi 14 adhabu ambayo ameimaliza.

Kwenye mechi ya jana ya watani, Zana ndiye
alianza kwenye kikosi cha kwanza huku
Boban na Banka walianzia benchi kuusoma mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa ndani na nje ya uwanja.

 Katika hatua nyingine, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harison Mwakyembe jana aliingia na staili yake uvaaji wa aina yake kwenye mechi hiyo kwa shati lake lilikuwa na rangi ya njano na nyekundu

Post a Comment

0 Comments