Windows

Makambo aachwa kwenye Orodha ya Wafungaji

Makambo aachwa kwenye Orodha ya Wafungaji

Wakati akionekana kustack na toka alipotoka kwao nchini Congo akiwa hajafunga bao lolote lile kwenye mchezo wa ligi kuu soka ya Tanzania bara TP Heritier Makambo wenzake wanaonekana magari yao kuwaka moto.


Heritier Makambo straika tegemezi zaidi kwenye kikosi cha Yanga mpaka sasa amesalia kuwa na magoli yake 11 huku siku ya jana akiachwa rasmi na mshambuliaji wa Mwadui Fc Salim Ayee ambaye alikuwa na magoli 10 na kufunga mawili na kufikisha magoli 12.


Salim Ayee msomaji wa Kwata Unit amekuwa moto ikiwa ni pamoja na kufunga Hat Trick kwenye mchezo mmoja ndiye anayeongoza kwa sasa akiwa na magoli 12 huku wanaomfuata akiwa ni Makambo wa Yanga mwenye jumla ya magoli 11 na wengine ni Eliud Ambokile Mbeya City,Said Dilunga wenye magoli 10.
Wengine wanaofuata baada ya wenye mabao 10 ni Dickson Ambundo wa Alliance na Meddie Kagere wa Simba wenye jumla ya mabao 9 mpaka sasa.

Post a Comment

0 Comments