Windows

MABAO NANE YAFUNGWA LEO TPL, MBILI ZABEBA POINTI TATU NA MBILI ZAGAWANA POINTI MOJA



LIGI Kuu Bara leo imeendelea huku jumla ya timu nane zikimaliza dakika tisini na kufanya jumla ya mabao nane kufungwa leo kwenye viwanja vitatu tofauti.

Timu mbili zimepata pointi tatu huku timu mbili zikigawana pointi mojamoja kama ifuatavyo:-

Zilizochukua pointi tatu

Mwadui FC wakiwa nyumbani Uwanja wa Mwadui Complex wamebeba pointi tatu mbele ya Biashara United kwa ushindi wa mabao 2-1.

Mabao ya Mwadui FC yamefungwa na Salim Aiyee dakika ya 45 na dakika ya 64 huku lile la Biashara United likifungwa na Wazir Jr dakika ya 50 kwa mkwaju wa penalti.

Lyon wakiwa nyumbani Uwanja wa Amri Abeid wanapoteza kwa kufungwa mabao 3-0 dhidi ya Simba.

Mabao ya Simba yamefungwa na John Bocco dakika ya 28 kwa penalti na dakika ya 46 huku bao la tatu akifunga Adam Salamba dakika ya 45.

Zilizogawana pointi mojamoja


Ruvu Shooting wamekubali kutoka suluhu nyumbani dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa Mabatini.

Coastal Union wakiwa nyumbani wanalazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Azam FC.

Bao la Coastal Union lilifungwa na Ayoub Lyanga dakika ya 45+2 na lile la Azam FC likifungwa na Obrey Chirwa dakika ya 52.

Post a Comment

0 Comments