Windows

KOCHA: YANGA ITAWASHANGAZA WENGI, KITAKACHOIPONZA SIMBA HIKI HAPA


BAADA ya kucheza na timu zote mbili Simba na Yanga na Yanga, kocha wa Stand United, Amars Niyoganbo amesema leo Yanga itawashangaza wengi.

Simba na Yanga zitamenyana leo Uwanja wa Taifa ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili wakiwa na kumbukumbu ya kutoka suluhu mchezo wao wa kwanza.

Niyoganbo amesema wengi hawaipi nafasi Yanga kutokana na mwenendo wake wa mechi za hivi karibuni ila wana kitu cha ziada ambacho kitawashangaza wengi.

"Naiheshimu timu ya Yanga, ni timu kubwa na ukitizama kuelekea kwenye mchezo wao wa watani wengi wanasahau kwamba Yanga inaongoza ligi kwa sasa hivyo sio ya kuibeza hata kidogo itafanya maajabu ambayo wengi hawatarajii.

"Uwezo na kasi yao uwanjani hasa kwa kuweza kubadili matokeo wana nafasi kubwa ya kufanya vizuri, kwa upande wa Simba kitakachowaponza kama watajiamini kupitiliza baada ya kumfunga mwarabu itakuwa ngumu kupata matokeo hivyo wasiibeze Yanga," amesema Niyogabo.


Post a Comment

0 Comments