NAHODHA wa Simba, John Bocco leo amewaongoza wachezaji wenzake kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa uwanja wa Mkapa.
Mchezo huu ambao ni kiporo cha mzunguko wa kwanza Simba wanafanikiwa kukimalizia vizuri licha ya ushindani walioupata kutoka kwa wapinzani wao Azam FC.
Bao la kwanza kwa Simba lilipachikwa kimiani na Meddie Kagere dakika ya nne baada ya mshambuliaji Emanuel Okwi kuachia shuti kali lililogonga mwamba na kurejea uwanjni kisha likakutana na kichwa cha Kagere.
Iliwalazimu Simba kusubiri mpaka dakika ya 39 kupachika bao la ushindi baada ya Simba kupata kona iliyoanzishwa na Okwi kisha akampa mzee wa kumwanga na kumimina maji Zana Coulibaly aliyeachia majalo yalikutana na kichwa cha Bocco.
Mpaka dakika 45 za mwanzo zinakamilika Simba walikuwa mbele kwa mabao 2 bila na kurejea kipindi cha pili ambapo tena iliwalazimu Simba kusubiri mpaka dakika ya 78 kupachika bao la tatu ambalo lilianzia kwa Clatous Chama kabla ya kumkuta Kagere ambaye alibabatiza mpira kisha akauzamisha nyavuni kwa mguu wake wa kulia.
Baada ya bao hilo alielekea kwenye goli akiwa na Dilunga, Zana kuutafuta mpira ulipopotelea.
Bao pekee la Azam FC walilipata kupitia kwa Frank Domayo aliyegonga bonge moja la shuti na kuingia ndani na ukarejea tena uwanjani akimalizia pasi ya Donald Ngoma.
Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi 45 ikiwa imecheza michezo 18 inabakiz pointi tano kuifikia Azam FC ambayo ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 50 huku mlima wa kuifikia Yanga ukibaki pointi 16.
0 Comments