

NAHODHA wa Yanga, Ibrahimu Ajibu alitumia dakika 61 kwenye mchezo wake dhidi ya Simba Uwanja wa Taifa kwa mara ya kwanza akiwa nahodha wa kikosi hicho kuongoza Kariakoo derby.
Ajibu ametwaa unahodha kutoka kwa Kelvin Yondani baada ya kocha Mwinyi Zahera kuamua kumvua kitambaa na kumpa Ajibu kwa kile alichoeleza ni utovu wa nidhamu.
Ikiwa ni mara yake ya kwanza kuongoza alitumia dakika 61 kucheza na kuongoza timu na ndipo kipindi cha pili dakika 61 alitolewa nafasi yake ikachukuliwa na Mohamedd Issa 'Banka'.
Kocha wa timu hiyo Mwinyi Zahera amesema kuwa alimtazama Ajibu muda mwingi akaona anapata taabu kwa mchezaji wa Simba mwenye nywele zenye rangi.
"Ajibu akiwa ndani ya uwanja alishindwa kuonyesha makali yake alikuwa anasumbuliwa sana na yule mchezaji wa Simba mwenye rangi kichwani (Zana Coulibary) hali iliyonishtua.
"Niliamua kumtoa ili kuongeza changamoto mpya kwani kama angeendelea kucheza ilikuwa ni hatari kwa timu yangu, tumepoteza hamna namna huu ni mpira," amesema Zahera.




0 Comments