

Baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 3-0 dhidi African Lyon hapo jana mkoani Arusha, kikosi cha Simba SC tayari kimerejea Dar es Salaam.
Wekundu hao wa Msimbazi wamerejea mapema ili kujiweka sawa zaidi na michezo ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (TPL) inayofuata.
"Kikosi chetu tayari kimerejea jijini Dar es Salaam, na leo jioni kitaanza mazoezi kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu," ameeleza taarifa kutoka ndani ya timu hiyo.
Baada ya ushindi wa hapo jana dhidi ya African Lyon, Simba SC wameweza kufikisha pointi 42 lakini wakiendelea kusalia kwenye nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi wakiwa wamecheza michezo 17. Wapinzani wao wa jadi Yanga SC wanaongoza Ligi hiyo wakiwa na Pointi 58 lakini wao wakicheza mechi 24.




0 Comments