

KUELEKEA kwenye mchezo wa kufuzu kushiriki michuano ya AFCON 2019, Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF) limetangaza majina 14 yatakayokuwa kwenye kamati iliyopewa jina la Saidia Taifa Stars ishinde.
Mwenyekiti wa kamati hiyo ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Katibu ni Mhandisi. Hers Said.
Wajumbe wengine ni pamoja na Mohamed Dewj 'Mo' Farouk Barhoza, Salim Abdallah, Patrick Kahemele na Abdallah Bin Kleb na Mohamed Nassor.
Wengine ni pamoja na Tedd Mapunda, Philimon Ntaihaja, Farid Nahid, Faraji Asas, Jery Muro na Haji Manara.
Stars watakuwa na kibarua mwezi Marchi kucheza na timu ya Taifa ya Uganda ili kufuzu hatua hiyo ya AFCON na dua zao zikiwa kwa Lesotho kupoteza mbele ya Cape Verde
Kwenye kundi L ambalo Stars ipo Uganda wamefuzu baada ya kufikisha pointi 13 huku Stars na Lestho zikiwa na pointi tano na Cape Verde wana pointi nne,




0 Comments