Baada ya kupoteza mchezo wa pili katika Ligi Kuu Bara hivi sasa, baadhi ya wanachama wa Yanga wameilalamikia Bodi ya Ligi ya TFF kwa kuchelewesha kutangaza majina ya waamuzi wa mechi ya watani.
Mwanachama anayejulikana kwa jina la Abdallah Chitemo, amesema Bodi ya Ligi inapaswa kumtangaza Mwamuzi walau siku 6 kabla kuelekea mechi hizo.
Wasiwasi wa Chitemo umekuja akieleza yawezekana kukawa na njama zinapangwa ili kuwaharibia Yanga makusudi kutokana na Bodi hiyo la Ligi kuchelewesha utangazaji wa Mwamuzi.
Ameeleza kuwa katika nchini zilizoendelea Mwamuzi hutangazwa mapema zaidi na akiwataka Bodi kujitathmini upya ili kuepuka lawama zisizo na msingi.
Katika mchezo uliopigwa Taifa jana, Yanga ilikubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Simba ambalo lilifungwa na Meddie Kagere kwenye dakika ya 71.
0 Comments