Windows

BAADA YA CHADEMA KWENDA FIFA, RAIS TFF AJA NA TAMKO HILI TENA


Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, Wallace Karia, amesema hajui kama CHADEMA wamepeleka barua FIFA baada ya kumtaja Tundu Lissu katika Mkutano Mkuu wa TFF uliofanyika jijini Arusha siku chache zilizopita, imeelezwa.

Taarifa inasema Rais huyo ameeleza kutokuwa na taarifa yoyote juu ya barua hiyo na akisema hajajua haswa kilichoandikwa nini ndani yake.

Katika Mkutano uliofanyika jijini Arusha, Karia aliwakemea baadhi ya viongozi ambao wanamuunga mkono Wambura pia akiwataja wale wenye tabia za ajabu kwa kusema 'Matundu Lissu' kitu ambacho CHADEMA kiliwakera.

Kutokana na kauli hiyo, CHADEMA iliamua kukaa chini na kuandika barua kutoka Idara ya Habari na Mawasiliano iliyo chini ya Tumaini Makene na kupelekwa FIFA huku nakala yake ikipitia Shirikisho la Soka Africa (CAF).

Baada ya CHADEMA kufanya maamuzi hayo, Karia aliamua kufunguka kwa kueleza hajui chochote na wala hawezi kuzungumzia suala lolote juu ya wao kwenda FIFA huku akieleza ufafanuzi alioutoa siku baada ya mkutano unatosha.

Post a Comment

0 Comments