Windows

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete yafikia mafanikio haya


Inaelezwa kuwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya kikwete (JKCI) imekuwa  ya kwanza Afrika Mashariki na Kati kuwa na wodi pekee ya kuwahudumia watoto wenye magonjwa ya moyo bila kuwachanganya na watu wazima.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamaii, Jinsi, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu ambapo ameeleza upatikanaji wa wodi hiyo ni juhudi za serikali katika kuhakikisha utolewaji wa matibabu ya moyo kwa watoto ya kibingwa yanaendelea kuboreshwa hapa nchini.

“Hapa Afrika Mashariki na kati hii ndio itakua wodi ya kwanza inayowahudumia watoto bila kuwachanganya na watu wazima na hii italeta ufanisi zaidi kwani nafasi ya kufanya makosa haitakuwepo kwasababu kutakuwa na wataalamu wanaohudumia watoto tu” alisema Waziri Ummy.

Aliendelea kwa kusema kuwa Serikali ilitoa Tsh. Milioni 700 kwa ajili ya ukarabati wa wodi hiyo na sasa kwa mara nyingine tena serikali imetoa Tsh. Milioni 500 kukamilisha miundombinu ya ukarabati.

Post a Comment

0 Comments