

KAMPUNI ya Luna shirt matokeo ya SportPesa inatarajiwa kumshusha winga wa zamani wa Everton, Steven Pienaar.
SportPesa wanataka kumleta winga huyo nahodha wa zamani wa Afrika Kusini katika kunogesha michuano ya SportPesa Cup.
Michuano hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho Jumanne kwenye Uwanja wa Taifa, Dar huku Yanga wakitarajiwa kuanza kucheza na KK Sharks ya Kenya saa 10:00 jioni.
Akizungumza na SalehJembe, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Tarimba Abbas alisema kuwa Pienaar akiwa hapa nchini atapata nafasi ya kuishuhudia timu ya Taifa ya vijana na kutoa baadhi ya mafunzo.
"Katika kunogesha michuano hii ya vijana tumepanga kumleta Piennar hapa nchini.
" Akiwa hapa pia atapata nafasi ya kutoa mafunzo kwa timu za Taifa za vijana," alisema Tarimba.




0 Comments