Windows

SMZ yasema inaendeleza kutekeleza azma ya kuwawezesha vijana


Waziri wa Kazi , Uwezeshji, Wazee, Wanawake na Watoto, Modiline Kastiko amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) itaendelea kutekeleza azma ya kuwawezesha vijana ili kuweza kujiajiri katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo na ufugaji.

kauli hiyo ameitoa wakati akimwakilisha Makamu wa Pili wa Rais katika Uzinduzi wa Ushirika wa Ufugaji kuku kwa vijana wa Mkoa wa Mjini Magharib,

Waziri Alisema miongoni mwa azma hizo ni kuhakikisha inatatua changamoto za ukosefu wa ajira kwa vijana kupitia wizara hiyo.

Ameongeza kuwa serikali imeona umuhimu wa kuanzisha wizara hiyo ili kuona vijana wanasaidiwa katika kuwatafutia mbinu mbalimbali za kuweza kijiajiri kwa lengo la kuondokana na vitendo viovu ambavyo vitawaharibia malengo yao ya maisha.

Waziri Castico amewataka vijana kuzitumia fursa hiyo ya mradi wa ufugaji kuku kwa lengo la  kujikwamua kiuchumi na  kuwawezesha vijana wengine kupata kuku hao na kuufanya mradi huo kuwa endelevu.

Castico amewataka vijana hao ambao wamepata mafunzo ya ufugaji wa kuku aina ya Saso kushirikiana na vijana wenzao kwa kuwapa elimu hiyo ili na wao waweze kufaidika na mardi huo na kuondokana na umasikini.

Kwa upande wake Msimamizi wa mradi huo, Rashid Mohamed amesema kuanzishwa kwa ushirika huo wa vijana wa ufugaji kuku mkoa wa Mjini Magharibi una lengo la kuhakikisha vijana wanajiongezea kipato na endelevu.

Pia amiomba serikali ya SMZ kuongeza nafasi za ajira kwa vijana wenye uwezo wa kufanya kazi kwa kuendeleza taifa .

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mahmud, alisema mradi huo utawasaidia vijana kujikwamua kiuchumi na kufikia uchumi wa kati.

"Mradii huu unatekelezwa kwa vitendo kwa kuwawezesha vijana kujiajiri wenyewe bila ya kutegemea ajira za serikali" alisema.



Post a Comment

0 Comments