Kocha wa AS Monaco ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa Arsenal Thierry Henryameomba radhi kufuatia kitendo chake kilicho naswa na Camera akitoa lugha ya kumtusi mchezaji wa Strasbourg Kenny Lala wakati wa mchezo dhidi yao uliyomalizika kwa AS Monaco kupoteza kwa kufungwa 5-1.
Thierry Henry alinaswa na Camera wakati wa mchezo huo dakika ya 43 akimtolea kauli Kenny Lala kwa kumtusi bibi wa mchezaji huyo kwani alimwambia mchezaji huyo “Bibi yako malay*” hata hivyo Henry baada ya kugundua kuwa alinaswa na camera za mchezo huo aliomba radhi wakati wa press conference na waandishi wa habari.

Kenny Lala aliyezungushiwa duara
“Ni kauli za mtaani bahati mbaya niliitamka najutia nichokifanya nikiwa benchi, ilikuwa ni muhemko tu wa kibinadamu na bado mimi ni muungwana najutia kwa hilo wakati mwingine huwa nafanya hivyo kwa kiingereza labda kwa kiingereza inaweza isitambulike, Hapana natania tu sikutakiwa kufanya hivyo”>>> Thierry Henry
Thierry mwenye umri wa miaka 41 ambaye ni miongoni mwa wachezaji wenye heshima kubwa katika club ya Arsenal anahesabika kama legend, kwa sasa ni kocha wa AS Monaco ya Ufaransa na ndio club yake ya kwanza kufanya kazi kama kocha mkuu na ana mtihani nayo wa kuhakikisha haishuki daraja kwani kwa sasa ipo nafasi ya pili kutoka mwisho ikiwa na point 15, ikipoteza michezo 13, sare 5 na imeshinda game 3.