

Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa ameivunja Bodi ya Mamlaka ya Maji Kibaigwa (KIBAWASA) kutokana na utendaji mbovu na kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kusambaza maji kwa wananchi katika mji mdogo wa kibaigwa.
Waziri Mbarawa amesema ameamua kuvunja bodi hiyo kutokana na kushindwa kufanya kutekeleza majukumu yake ikiwamo kumshauri Meneja wa Kibawasa katika majukumu yao.
“Kuanzia leo navunja bodi hii kwa sababu imeshindwa kutekeleza majukumu yao na kusababisha kukosekana kwa maji katika Mji huu, nahii ndio inasababisha hadi Meneja wa KIBAWASA kushindwa kutekeleza majukumu yake kutokana na kutoshauriwa na bodi hii” alisema Waziri Mbarawa.
Waziri Mbarawa alifanya ziara yake katika Wilaya ya Kongwa na Chamwino Mkoani Dodoma kwa lengo la kukagua miradi ya maji inayotekelezwa na Serikali na kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji kwa wananchi.



0 Comments