Uongozi wa timu ya Yanga umesema kuwa bado suala la mlinda mlango, Beno Kakolanya linashughulikiwa na wanasheria ili kuweka mambo sawa.
Kaimu Mwenyekiti wa klabu hiyo Samwel Lukumay amesema walikuwa wanashughulika tatizo la Kakolanya ambaye alishindwa kujiunga na timu msimu huu wakati timu inakwenda kucheza na Mwadui ya Shinyanga.
“Kakolanya alishindwa kujiunga na timu wakati tunakwenda kucheza na Mwadui na mwenzake Kelvin Yondani ila Yondani alirejea yeye akashindwa kurejea zaidi ya kutuandikia barua ya kuomba alipwe stahiki zake na kusitisha mkataba na timu.
“Baada ya mazungumzo tulikubaliana tumlipe stahiki zake ili arejee ndani ya timu ila hakuweza kufanya hivyo baada ya kuanza kulipwa stahiki zake bila kutoa taarifa yoyote, hali iliyopelekea kocha mkuu Mwinyi Zahera kumkataa.
“Tarehe 25 alituandikia barua nyingine kupitia kwa mwanasheria wake akihitaji kuvunja mkataba wake na ilikuwa ni barua ya msisitizo ambayo tuliipokea tarehe 28 hivyo kwa sasa bado tunaendelea kuitendela kazi kwa kuwa ni masuala ya kisheria,” alisema Lukumayi.
0 Comments