Straika wa Simba, Mnyarwanda Meddie Kagere amefunguka kwamba kipigo walichopokea kutoka kwa AS Vita kinabaki kama historia na sasa wanageukia kuutazama kwa umakini mchezo wao na Al Ahly.
Simba juzi Jumamosi walipoteza mchezo wao wa pili wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika mbele ya AS Vita kwa kufungwa mabao 5-0 nchini DR Congo.
Straika huyo mwenye mabao matano kwenye Ligi ya Mabingwa msimu huu, amesema kwamba kwa sasa wanachokitazama mbele ni namna gani watashinda mechi yao ijayo na Al Ahly na siyo kuanza kufikiria tena juu ya kipigo cha Vita.
“Tunaangalia mechi kwa mechi, pale tukimaliza moja ndiyo tunatazama nyingine tutafanya nini, hatuwezi kuangalia mechi zote kwa wakati mmoja.
“Tumeshamaliza mechi hii iliyopita na inabaki kama historia, kwa sasa lengo lililo mbele ni kushinda mchezo ujao dhidi ya Al Alhy,” alisema Mnyarwanda huyo.
Simba wanaofundishwa na Mbelgiji Patrick Aussems watasafiri kuwafuata Al Ahly nchini Misri na kucheza nao Februari 2, mwaka huu.
0 Comments