Windows

Huyu ndiye Mtanzania aliyefanya kweli FA Cup nchini England, ashika nafasi ya pili kwa kupachika mabao

Michuano ya kombe la FA Cup nchini England inatarajiwa kuendelea tena hii leo siku ya Ijumaa ambapo Arsenal itaivaa Manchester United.


Wakati vigogo hao wa soka wakitarajiwa kujitupa uwanjani hapo baadae, upande wa pili kuna Mtanzania anayeshika nafasi ya pili kwa ufungaji mabao katika michuano hiyo.
Huwenda Watanzania wengi hawafahamu hilo, lakini ndiyo uhalisia Straika huyo wa Tanzania mwenye umri wa miaka 26, Adi Yussuf ambaye anaitumikia klabu ya Solihull Moors inayoshiriki ligi daraja la tano England maarufu kama National League.

Image result for adi yussuf solihull moors fa cup

Yussuf siyo maarufu sana kwenye soka la Tanzania lakini amewahi kuitwa ili kuitumikia Taifa Stars wakati huo akiwa anaichezea Mansfield Town iliyokuwa ligi daraja la tatu England.
Mshambuliaji huyo aliyezaliwa Tanzania kabla ya wazazi wake kuhamia England ambako ndiko alikokulia, amekuwa mshambuliaji tegemeo katika timu hiyo.


Licha ya kuwa timu yake imeshatolewa kwenye michuano hiyo ya FA Cup amefanikiwa kufunga jumla ya mabao matatu na hivyo kuwa nafasi ya pili na kuwa nyuma ya vinara kadhaa wanaoshika nafasi ya kwanza wakiwa na mabao manne kila mmoja.
Kijana huyo ambaye inaelezwa kuwa baba yake aliwahi kuichezea Coastal Union ya Tanga, hakupata nafasi nzuri ya kuichezea Taifa Stars kwa kuwa wakati alipoitwa mwaka 2016 aliandamwa na majeraha na hivyo kukosa nafasi nzuri ya kuliwakilisha Taifa lake alikozaliwa.
Timu ya Adi Yussuf ilianza mzunguko wa kwanza kwa kucheza dhidi ya Hitchin Town ambapo walishinda kwa jumla ya mabao 2 – 0 ilikuwa Novemba 11 mwaka 2018 huku Mtanzania huyo akifunga bao moja kwa penati katika dakika 72 na kufanikiwa kusonga mbele.
Kwenye mzunguko wa pili wa kombe hilo Novemba 30, Solihull Moors FC walikutana na Blackpool ambapo katika mchezo wa awali ambapo ulimalizika kwa sare ya 0 – 0.
Katika mchezo wa marudiano Desemba 18, timu hizo zilirudiana na ndipo wakatolewa kwa jumla ya mabao 3 – 2 kwenye dakika za nyongeza baada ya matokeo ya 2 – 2 ndani ya dakika 90. Ambapo Yussuf alifunga mabao yote mawili dakika ya 33 na 51 kabla ya Blackpool kupata bao la ushindi kwenye dakika 105.




Adi Yussuf anashika nafasi ya saba kwenye msimamo wa wafungaji kunoka ligi ya National League baada ya kujikusanyia jumla ya mabao tisa huku nafasi ya kwanza ikiongozwa na Danny Rowe mwenye jumla ya magoli 19.

Post a Comment

0 Comments