MSHAMBULIAJI wa Simba, Emanuel Okwi ameweka rekodi mpya Uwanja wa Taifa kwenye michuano ya SportPesa Cup hatua ya robo fainali kwa kuisaidia timu kutinga hatua nusu fainali kwa ushindi wa mabao 2-1 akiwa nahodha.
Okwi amekuwa nahodha wa kwanza kwenye michuano ya SportPesa Cup kutoa pasi na kufunga kwenye mchezo wa robo fainali waliocheza dhidi ya AFC Leopards ya Kenya.
Kwenye mchezo huo alifunga bao dakika ya 13 akimalizia pasi ya Zana Coulibaly na kuifanya Simba kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili dakika ya 47 Okwi alitoa pasi ya bao Clatous Chama alikomelea msumari wa ushindi.Dakika ya 52 alipata kadi ya njano kutokana na kumchezea rafu mchezaji wa AFC Leopards alitoka dakika ya 66 nafasi yake ikachukuliwa na Mzamiru Yassin.
0 Comments